Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:19

Mapigano mapya yazuka Somalia


Mapigano mapya yamezuka katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu jana Jumanne, na kuuwa watu wane na kuwajeruhi watu wapatao 20 wengine.

Mashahidi wanasema majeruhi wengi walitokea katika eneo la soko la Bakara, kaskazini mwa wilaya ya Hawl Wadaag huko Mogadishu. Mapigano yanaonekana kuwahusisha waasi na majeshi ya serikali ambayo yamekuwa yanapigana kuudhibiti mji mkuu.

Serikali dhaifu ya Somalia, inazidi kupata shinikizo la kuchukua hatua kali dhidi ya wanamgambo wa ki-Islam hasa al-Shabab. Kundi hilo la uaso linaaminika kuwa na ushirikiano na wanamgambo wa al-Qaida.

XS
SM
MD
LG