Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:42

Rais wa Angola aelezea umaskini nchini mwake


Rais wa Angola anasema robo tatu ya watu nchini mwake wanaishi katika hali ya umaskini, na kwamba chama tawala cha Popular Movement for the Liberation of Angola-MPLA, lazima kifanye kazi zaidi kuwasaidia watu hao.

Rais Jose Eduardo dos Santos alizungumza jana Jumatatu kwenye bunge la taifa la MPLA, katika mji mkuu, Luanda. Alisema kwa kila wa-Angola 100, 60 ni maskini sana, kwa maneno yake hawawezi kula mlo wa kawaida kila siku. Aliongeza kwamba wengi pia hawana fursa ya kupata maji ya kunywa, huduma za afya na makazi ya kawaida. Rais alisema juhudi za chama zinatakiwa kulenga kutokomeza umaskini, kutojua kusoma na ukosefu wa ajira.

Kiwango cha juu cha umaskini kimekuwepo kwa muda mrefu licha ya ongezeko la uzalishaji mafuta tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002 ambavyo vilidumu kwa miaka 27 nchini Angola. Bwana Dos Santos ambaye ameongoza Angola kwa miaka 30, pia alirudia wito alioutoa mwezi uliopita kumaliza rushwa iliyozagaa nchini kote.


XS
SM
MD
LG