Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 09, 2024 Local time: 18:58

Rais Umaru Yar'Dua wa Nigeria, kwenda Saudi Arabia kwa matibabu


Rais wa Nigeria Umaru Yar’Adua anakwenda Saudi Arabia jumatatu kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.

Ofisi ya rais imesema bwana Yar’Adua anatarajiwa kumpigia simu daktari wake binafsi katika mji wa Jeddah, kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Bwana Yar’Dua ana ugonjwa sugu wa figo na amewahi kwenda Ujerumani na Saudi Arabia mara nyingi miaka mitatu iliyopita kwa ajili ya matibabu kiafya.

Wakosoaji wameuliza kama rais huyo mwenye umri wa miaka 58 ana uwezo wa kiafya kuongoza taifa hilo maarufu katika bara la Afrika.

Hii itakuwa mara ya tatu kwenda Saudi Arabia tangu mwezi Augosti.

XS
SM
MD
LG