Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 01:18

Msichana wa Miaka Minane Abakwa Marekani


Polisi katika jimbo la mji wa Phoenix ulioko jimbo la Arizona kusini magharibi mwa Marekani,wamewakamata wazazi wa msichana wa miaka minane mzaliwa Liberia aliyedaiwa kubakwa na wavulana wanne.

Mamlaka zinasema kuwa wazazi wa msichana huyo wanakabiliwa na mashitaka ya kumwachia ovyo huyo na kumtesa kwa miaka mingi. Polisi wa mji wa Phoenix wanasema wazazi wa msichana huyo walikamatwa jana ijumaa.

Msichana huyo amepelekwa katika kituo cha malezi baada ya kubakwa mwezi Julai na wavulana wanne kutoka Liberia wenye umri wa miaka 10, 13 na 14.
Babake msichana huyo alinukuliwa akisema kuwa hamtaki tena mwanawe,kwa sababu ameiletea familia yake aibu kubwa.

XS
SM
MD
LG