Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 19:36

Marekani yazungumzia ugaidi Afrika


Marekani inasema inaangalia kwa makini vitisho kutoka al-Qaida tawi la Afrika kaskazini kwenye eneo la jangwa la Sahara barani Afrika.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulika na masuala ya Afrika Johnnie Carson aliliambia baraza la Seneti Jumanne, kuwa zaidi ya miezi sita iliyopita, al-Qaida ya eneo la kaskazini-magharibi ya Afrika imehusika na mauaji ya mfanyakazi mmoja wa kutoa msaada raia wa Marekani, afisa mmoja mwandamizi kutoka Mali na lilifanya jaribio la bomu la kujitoa mhanga kwenye ubalozi wa Ufaransa huko Mauritania.

Carson anasema Marekani ina nia ya dhati kusaidia nchi zilizopo kwenye eneo la Sahel ikiwa ni pamoja na nchi za Sudan, Eritrea, Chad, Senegal, Niger, Nigeria, Algeria, Mauritania na Mali kupambana na ugaidi.
Afisa mmoja wa Marekani katika idara ya maendeleo ya kimataifa-USAID, akizungumza kwenye baraza hilo la Seneti, alisema program za idara yake katika eneo hilo zinalenga kuboresha nafasi kwa vijana, ambao anasema wanaonekana kupatiwa mafunzo na makundi ya kigaidi.

Mwaka 2005, utawala wa Bush ulianzisha ushirikiano wa Trans-Sahara wa kupambana na ugaidi, kuongeza uwezo wa serikali za huko kupambana na ugaidi, pamoja na nchi za Algeria, Morocco na Tunisia.

XS
SM
MD
LG