Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 11:57

Chama cha Bemba DRC chaelekea kugawanyika


Chama kikuu cha upinzani nchini DRC kinaelekea kusambaratika kufuatia tofauti zilizopo baina ya viongozi wake. Uchaguzi wa gavana wa mkoa wa Equatear utakaofanyika Ijumaa ambao ndio ngome ya upinzani unasababisha mpasuko mkubwa baina ya wanachama wa chama kinachoongozwa na Jean Pierre Bemba ambaye hivi sasa amefungwa huko The Hague.

Baadhi ya vigogo wa chama hicho wamejitoa na wengine wametengwa na chama kwa sababu ya mtazamo wao tofauti na kuweka ishara za wazi ndani ya chama hicho ambazo zimejidhihirisha wiki hii kufuatia kampeni za uchaguzi wa gavana huko kaskazini-magharibi mwa Congo.

Chama hicho kilishindwa kufikia muafaka kuhusu mgombea wa chama kwenye kiti hicho cha gavana na kupelekea kuwepo wagombea wanne wote kutoka chama hicho, na katibu mkuu wa MLC ambaye hivi sasa anaongoza chama hicho Francis Mwamba, anasema mgombea wa chama ni mbunge Jean Lisie Musa.

XS
SM
MD
LG