Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:52

WHO: wanawake wabaguliwa kupata huduma za afya


Ripoti chungu nzima zimeandikwa hasa kuhusiana na masuali ya afya yanayao waathiri wanawake, kama matatizo katika huduma za uzazi. Lakini hii ni mara ya kwanza kwa utafiti kuchunguza kwa mapana na marefu mahitaji na matatizo ya afya yanayowathiri wanawake mnamo uhai wao.

Wakichunguza kutokana na muangalio huo, ripoti imegundua kwamba jamii imeshindwa kukabiliana na mahitaji ya huduma za afya ya wanawake katika wakati muhiumu ya maisha yao, hasi wakati wa miaka ya utotoni na uzeni.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Magaret Chan, alitaja kasoro hizi zinatokana na sababu msingi zenye utata mkubwa. Lakini alisema uchambuzi wa takwimu katika utafiti unaonesha kuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya ubaguzi dhidi ya wanawake na afya dhaifu.

Anasema, “kile ripoti hii imepima ni athari za kina ambazo hadhi ya kijami inasababisha katika afya ya wanawake na wasichana. Kama ripoti inafafanua kwamba, vizuizi vinavyo zuia wanawake kupata huduma bora za afya siyo ufundi au tiba yenyewe bali ni masuala ya kijami na kisiasa na zote mbili zinambatana.”

Chan anasema hakutakua na maendeleo muhimu kwa upande wa afya ya wanawake ikiwa wataendelea kuchukuliwa kua raia wa tabaka la pili katika sehemu nyingi za dunia.

Ripoti ya WHO inadokeza kwamba, wanawake wanazaliwa na nafasi nzuri ya kibiolojia, ya kuishi miaka sita hadi minane zaidi kuliko wanaume. Lakini hiyo haimanisha kua na maisha ya furaha.

Ripoti inagundua wanawake wana uwezo mkubwa wa kupatwa na wasi wasi na unyonge kuliko wanaume na inakadiriwa kwamba wanawake milioni 73 kote duniani wanakabiliwa na hali kuu ya unyonge takriban kila mwaka.

Ripoti inalinganisha afya ya wanawake katikia mataifa tajiri na maskini ambayo Bi Chan ansema siyo kwa sababu ni wanawake mambo ni tofauti.

Anasema, “tofauti zilizopo katika sababu kubwa ya vifo na ulemavu katika makundi hayo mawili ni kubwa sana. Mwanamke katika nchi ya Afrika kusini mwa janga la Sahara anakabiliwa na hatari mara saba zaidi ya kufa kuliko mwanamke katika nchi tajiri.”

Ripoti inaeleza kote duniani wanawake ndiyo wanaotoa sehemu kubwa kabisa ya huduma za afya ikiwa ni majumbani mwao, jamii au mfumo wa afya. Lakini inapohusu huduma za afya kwa wanawake ripoti inagundua mfumo unashindwa kukabiliana na mahitaji maalum na changamoto zinaozwakabili wanawake maishani mwao yote.

XS
SM
MD
LG