Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:45

Kampeni za uchaguzi mkuu Msumbiji za pamba moto


Wagombea kiti cha urais nchini Msumbiji wamefanya kampeni zao za mwisho kabla ya upigaji kura siku ya Jumatano. Wagombea wote watatu walimaliza kampeni zao Jumapili, wakiwasihi wafuasi wao kujitokeza kupiga kura.

Uchaguzi unatarajiwa kumpatia ushindi Rais Armando Guebuza, ambaye anakabiliana na mgawanyiko wa upinzani. Wapinzani wake ni Afonso Dhlakama, kiongozi mkuu wa chama cha upinzani cha Renamo, na Daviz Simango, mwanzilishi wa chama kilichojitenga cha Democratic Movement of Mozambique.

Simango alijitoa kutoka chama cha Renamo mwanzoni mwa mwaka huu, na kuwachukua maafisa wakuu wa upinzani. Upigaji kura wa Jumatano utachagua pia viongozi wa bunge na majimbo.

Chama tawala cha Frelimo kimeongoza Msumbiji tangu ilipopata uhuru wake kutoka Ureno mwaka wa 1975.


XS
SM
MD
LG