Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 30, 2022 Local time: 00:38

Jumuia ya kimataifa haiwasaidi IDP's wa Somalia


Mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya haki za watu waliokoseshwa makazi ndani ya nchi, Walter Kalin amehitimisha ziara ya wiki moja kulitembelea eneo hilo akilenga hali ya wakimbizi wa ndani nchini Somalia.

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa alitoa ombi kwa dunia kuongeza mara mbili juhudi za kuwasaidia wale ambao wamelazimika kukimbia nyumba zao nchini Somalia.
“Jumuiya ya kimataifa kwa kiasi kikubwa imeshindwa kuwahudumia watu waliokoseshwa makazi nchini Somalia.”

Idadi ya wasomali wanakimbia mapigano kati na kusini mwa Somalia, ambako wanamgambo wanaoipinga serikali wanajaribu kuiangusha serikali ya Mogadishu inayoungwa mkono na Jumuia ya Kimataifa. Sehemu kubwa ya nchi inadhibitiwa na wapiganaji wa waasi.

Wilaya nje ya Mogadishu, inayojulikana kama Afgooye, ina idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani hapa duniani. Ingawa Bw. Kalin hakuitembelea Somalia kusini na ya kati, kutokana na sababu za usalama alikutana na wale ambao wamekimbia maeneo yao. Walielezea kusambaa kwa ghasia dhidi ya raia na hali mbaya katika kambi za IDP’s.

Kalin alizishutumu pande zote katika mzozo huo kwa kutenda ukatili dhidi ya raia na kukiuka sheria za kimataifa. Alisema, hali ya kibinadamu katika makambi za muda - nyingi zikiwa si rahisi kufikiwa na mashirika ya kimataifa ya misaada - haikubaliki hata kidogo.

Alisema kambi zina ukosefu wa huduma za msingi kama vile chakula na maji, makazi ya kutosha na huduma za afya, na kuelezea kusambaa kwa vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake na wasichana. Zaidi ya watu milioni moja na nusu Somalia wanaaminika walokimbia makazi yao.

Marekani ilitangaza inashikilia shehena ya misaada ya dola milioni 50 kwa Somalia wakati inatafuta mbinu za kugawa misaada. Mamlaka ya usalama ina wasi wasi kwamba baadhi ya misaada inaangukia kwenye mikono ya kundi la wanamgambo la Al-Shabab lenye uhusiano na Al-qaida, kundi ambalo linakiuka sheria za Marekani dhidi ya ugaidi.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa pia aliyataka mashirika ya misaada yenye makao yake Nairobi kuhamishia operesheni zao katika mikoa ya kaskazini mwa Somalia ya Somaliland pamoja na Puntland ambako hali si mbaya sana.

Ziara ya Bw Kalin unafanyika kabla ya kuanza mkutano nchini Uganda kuzungumzia haki za wakimbizi wa ndani ambao hivi sasa hawatambuliwi sana kuliko wakimbizi wengine.

XS
SM
MD
LG