Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 09:11

Afrika Mashariki yazidi kukumbwa na njaa


Takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na utafiti wa kilimo na chakula duniani, zinaonesha idadi ya mataifa yanayokabiliwa na upungufu wa chakula katika mataifa ya Afrika kusini mwa jangwa la sahara inazidi kuongezeka. Katika nchi za Afrika mashariki tatizo hilo limesababishwa na ukame wa muda mrefu, hali mbaya ya umasikini, kudorora kwa uchumi duniani na migogoro ya kisiasa.

Taarifa zinasema hali ya chakula inazidi kutatanisha na viwango vya njaa katika nchi hizo vinasababisha wasi wasi mkubwa, kwa nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Eritrea, Ethiopia na Somalia na hali mbaya ya ukame inaendelea kuathiri sana raia wa nchi hizo.

Kulingana na utafiti huo jambo la kusikitisha zaidi ni kuendelea kwa hali hii ya ukosefu wa chakula hadi mwezi Machi mwaka ujao. Shirika hilo linasema hata biashara ya utalii katika nchi hizo inaendelea kuathirika sana kutokana na kufa kwa wanyama pori pamoja na mifugo kwa ujumla.

XS
SM
MD
LG