Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 08:13

Dunia yamkumbuka Mwalimu


Wakati Tanzania inadhimisha miaka kumi tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere tarehe 14 Oktoba mwaka 1999, watanzania na ulimwengu mzima wanatoa maoni na hisia mbali mbali juu ya mchango wake na jinsi taifa lilivyo hii leo.

Wasomi na wanasiasa pamoja na wananchi wanamueleza Mwalimu kua alikua kiongozi aliyetetea maslahi ya taifa lake na wananchi wake, jambo ambalo halipatikani miongoni mwa viongozi wa leo.

Profesa Issa Shivji, mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salam, ameimabia Sauti ya Amerika kwamba cha ajabu ni kua mwaka huu kinyume na miaka ya nyuma, vyombo vya habari na wachambuzi wameanza kumzungumzia na kumjadili Mwalimu hasa katika sera zake za Azimio la Arusha.

"Kwa kweli kulikua na wakati ambapo watu walikua wanamzungumzia Mwalimu Nyerere bila ya kutaja Azimio la Arusha. Mimi ninaona hii ni muhimu sana na hii inaonesha kwa kiasi gani mfumo na sera zilizofuatwa baada ya yeye kun'gtuka, kwa kweli zimeonesha zimefilisika."

Salim Ahmed Salim, mwenyekiti wa taasisi ya Mwalimu Nyerere, anasema kwa ujumla mambo yale Mwalimu aliyapigania na kuyashikilia sana ni mambo yanaokumbukwa hasa na wananchi wa kawaida.

"Suala na unyonyaji wa mataifa makubwa kwa mataifa madogo linakumbukwa na wananchi wa kawaida wa Tanzania na linakumbukwa pia na wananchi wa Afrika. Ukweli ni kwambaj ambo hili limendelea na hasa katika dunia hii ya leo ya utandawazi, na matatizo yake na changamoto zake, watu wanakumbuka sana jinsi Mwalimu Nyerere alivyopigania haki za nchi changa kama Tanzania, kwa kuhakikisha kwamba angalau sisi tunapata haki katika jamii ya Kimataifa."

XS
SM
MD
LG