Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 02, 2022 Local time: 15:56

Annan aridhika na mazungumzo yake Kenya


Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan amekamilisha ziara yake ya siku nne huko Kenya, kwa kukutana tena na Rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Riala Odinga.

Akizungumza na waandishi habari kabla ya kuondoka alisema viongozi wa Kenya wamemuahidi kuendelea na utekelezaji wa makubaliano yaliyo pelekea kuundwa kwa serekali ya mseto.

Hata hivyo Bw Anna aliwaonya viongozi hao kwamba muda wa kutekelza mageuzi unakimbia na kunahaja ya dharura kuepusha kutokea ghasia kama zilizotokea wakati wa uchaguzi ulopita.

Mpatanishi huyo mkuu anaondoka wakati kuna ripoti kwamba wa Kenya wameanza kujihami kwa kununua silaha kabla ya uchaguzi wa 2010. Inaripotiwa kwamba watu hivi sasa wananunua bunduki za kila aina ili kuweza kujikinga pindi patatokea ghasia.

XS
SM
MD
LG