Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 08, 2024 Local time: 18:58

Wazir Wetangula akutana na balozi wa Marekani


Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Moses Wetangula, alikutana Jumanne na Balozi wa Marekani nchini Kenya, Michael Ranneberger kuwasilisha malalamiko ya serekali.

Wetangula alimkabidhi balozi huyo malalamiko kuhusu barua 15 walizopelekewa mawaziri na watu wengine mashuhuri wakijulishwa kuwa huenda wapigwe marufuku kukanyanga ardhi ya Marekani ikiwa wataendelea kupinga mageuzi ya kisiasa kati ya mageuzi mengine muhimu nchini humo.

Vyanzo vya serekali ambao hawakutaka kutaja majina yao wameiambia sauti ya amerika kuwa katika mkutano wake na balozi Ranneberger, Bw Wetangula, alieleza kukerwa kwa wakuu wa serekali kutokana namna barua hizo zilivyotolewa.

Kwa upande wake, balozi wa Marekani alishikilia msimamo wake thabiti kuwa, serikali ya Marekani ilituma barua hizo kwa waliohusika kutokana na sababu kwamba eti walizuia kufanyika kwa mageuzi ya kisiasa, marekebisho ya katiba, uhakikisho wa usawa wa sheria za nchi, hatua madhubuti kukomesha ufisadi, marekebisho yanayohusika na umiliki wa ardhi na uwazi na utendaji wa haki kuhusu waliohusika na fujo zilizosababisha maafa baada ya uchaguzi ulioleta utata wa mwaka 2007 na mengine muhimu yaliyoahidiwa kufanywa na serikali ya Kenya.

Marekani pia ilidai kuwa mawaziri hao na wengineo, walieneza ndimi za kuchochea mapigano ili waweze kujinufaisha na kujidumisha kisiasa.

Hata hivyo, balozi wa Marekani na Waziri Wetangula hawaakutangaza kinaganaga undani au maafikiano ya mkutano wao.

Mapema Wetangula alipokutana na waandishi wa habari katika ofisi zake huko Nairobi, alieleza kwamba kitendo hicho ni ukiukaji wa itifaki za kidiplomasia.

Ingawaje Waziri Wetangula anasema kuwa si sawa kwa Wakenya kuandikiwa barua, balozi Ranneberger anashikilia kikamilifu kuwa kuandikiwa kwa barua hizo ni sawa.

Balozi huyo anasema kuwa licha ya sakata ya barua hizo kwa Wakenya 15, uhusiano kati ya Kenya na Marekani bado uko imara daima na kwamba kamwe hauwezi kuharibika.

XS
SM
MD
LG