Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 23:13

Watu wanane wafariki kutokana na mafuriko Atlanta


Mvua kubwa zilizonyesha katika majimbo ya Kusini mwa Marekani kwa wiki nzima zimeleta maafa makubwa na kusababisha vifo vya watu wanane huko jimbo la Atlanta na wengine kadhaa kupoteza makazi yao.

Akizungumza na sauti ya Amerika mwandishi BMJ Murithi anayeishi huko Atlanta Georgia alielezea kuwa mvua hizo zimepelekea maafa makubwa na madhara si Atlanta tu bali pia kwenye maeneo katika majimbo mengine ya karibu kama vile North Carolina, Tenesee, Alabama na Kentucky.

Ni mafuriko ambayo baadhi ya watu wanasema hayajaonekana kwa muda mrefu. Naye Gavana wa jimbo la Georgia Sonny Perdue ametangaza hali ya tahadhari na kusema kwamba serikali itafanya juu chini kuhakikisha kwamba waathiriwa wanapata msaada unaostahili. Mashule na biashara yamefungwa.

XS
SM
MD
LG