Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 08:37

UN yazungumzia wanajeshi watoto katika maeneo ya vita


Mwakilishi maalum wa umoja mataifa kwa masuala ya watoto na mizozo ya silaha anasema mwaka uliopita umekuwa mbaya kwa watoto katika maeneo yaliyokumbwa na vita. Katika ripoti iliyowasilishwa kwa baraza la haki za binadamu la umoja mataifa, mwakilishi maalumu anaelezea hali mbaya ya wanajeshi watoto na watoto wengine katika mizozo kadhaa kote duniani.

katika maelezo yenye matumaini, umoja mataifa inakadiria idadi ya wanajeshi watoto duniani imeshuka mpaka laki mbili na elfu hamsini ukilinganisha na laki tatu miaka mitano iliyopita.

Mwakilishi maalumu wa umoja mataifa Radhika Coomaraswamy anasema katika kipindi cha mwaka uliopita, idadi kubwa ya wanajeshi watoto waliachiwa huru na National Liberation forces nchini Burundi na watoto zaidi wanatarajiwa kuachiwa huru katika Jamhuri ya Afrika ya kati na phillipines, ikiwa ni matokeo ya hatua za haraka za umoja mataifa kuingilia kati.

Lakini kwa sehemu kubwa, anasema kuna maendeleo yasiyo na matumaini ambayo yanachukua nafasi ya yale yenye matumaini. Coomaraswamy anaelezea matatizo ya wanajeshi watoto katika maeneo yenye mizozo huko Gaza, Sri Lanka, Pakistan, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Irak na Afghanistan.

Katika mizozo yote hiyo, anasema wanajeshi watoto na watoto wengine wameathirika ni kiwango kikubwa cha majeruhi na ukiukaji mkubwa. Wengi wamekuwa wakimbizi wa ndani ya nchi.

Anasema hali ya watoto katika kambi huko Sri Lanka ni ya kutia wasi wasi mkubwa.

Katika ripoti yake kwa baraza la haki za binadamu la umoja mataifa, mwakilishi maalumu anachambua matukio mabaya ya ukiukaji dhidi ya watoto huko Gaza, akielezea kile walichoathiriwa kiasi kwamba hawawezi kuelezea.

Anasema mapigano kati ya serikali na makundi ya uasi ya wahutu katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo yamesababisha watoto wengi kuuwawa na kukatwa viungo.

Anasema watoto wengi katika jimbo la North West Frontier huko Pakistan wanalazimishwa kunadikishwa na wanamgambo na kupatiwa mafunzo ya kuwa wapelelezi, wapiganaji au walipuaji mabomu wa kujitoa mhanga.

Coomaraswamy anasema pia anawasiwasi mkubwa kuhusu mabadiliko ya mazingira ya mgogoro, hasa katika mapambano kati ya ugaidi na kukabiliana na ugaidi.

Coomaraswamy anasema ni muhimu sana kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kujizatiti na kuwafuatilia wale ambao wanakiuka haki za watoto wawajibishwe. Anasema wale waliohusika kwenye uhalifu wanatakiwa wa-adhibiwe.

XS
SM
MD
LG