Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 02:09

Kenya Yakumbwa na Upungufu wa Chakula.


Serikali ya Kenya imeanza kubuni njia mpya za kuimarisha utoaji wa nguvu za umeme kufuatia upungufu mkubwa wa maji na pia baadhi ya maeneo ya nchi yakikabiliwa na uhaba wa chakula.

Kwa mwaka wa pili mfululizo hali mbaya ya kiangazi nchini Kenya imeathiri watu milioni kumi ambao wanakabiliwa na janga la njaa na wanahitaji msaada wa haraka wa chakula. Waziri mkuu wa Kenya, bwana Raila Odinga amelazimika kuwasilisha suala hili katika bunge la taifa.

Kwa mujibu wa taarifa ya serikali Kenya ina upungufu wa zaidi ya magunia milioni 13 ya mahindi.Serikali imeanza mipango ya kuagiza chakula kutoka nje ili kukidhi mahitaji ya ndani ya nchi.

Hali hii imekuwa mbaya zaidi hasa katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa nchi ambayo yamekumbwa na ukame wa muda mrefu. baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wameanza kupika mizoga ya punda kutokana na uhaba wa chakula.

XS
SM
MD
LG