Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 29, 2020 Local time: 22:36

Tume ya Uchaguzi Iran kuchunguza matokeo


Baraza la Walinzi wa Mapinduzi la Iran limetangaza kwamba liko tayari kuhesabu upya kura za uchaguzi wa rais wenye utata mkubwa ambapo rais Mahamoud Ahmedinejad alitangazwa mshindi.

Mgombea mashuhuri mpenda mageuzi Mir Hossein Mousavi anayepinga matokeo hayo, alikutana na wajumbe wa baraza hilo ili kujadili juu ya kuhesabiwa upya kura. Mgombea huyo wa upinzani alijadili na wajumbe wa baraza hilo ambalo ndilo linasimamia uchaguzi nchini humo, juu ya utaratibu wa kuhesabu upya kura kutokana na uchaguzi wa Ijumaa.

Tume ya uchaguzi ilidokeza mapema kwamba iko tayari kuhesabu upya kura zilizosababisha mabishano makubwa nchini humo, baada ya rais Ahmedinejad kutangazwa mshindi, kukiwepo na malalamiko ya wizi kutoka upinzani.

Akizungumza na televisheni ya taifa kiongozi wa baraza, Ayatollah Ahmed Jannati alisema, baraza lake liko tayari kuchunguza upya matokeo ya uchaguzi huo.Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG