Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:38

Bajeti za Afrika Mashariki


Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati ya Kenya, Tanzania, Uganda na Rwanda yametangaza bajeti za mwaka mpya wa fedha wa 2009-2010 zikiwa na ongezeko kubwa la matumizi kwa nchini zote. Bajeti ya Kenya imetangaza matumizi ya Sh. Billioni 867, ikiwa ni matumizi makubwa kuliko yote katika historia ya nchi hiyo. Sehemu kubwa ya fedha hizo zitatumiwa katika elimu, Ulinzi na Usalama na Ujenzi wa barabara. Nchini Tanzania, serikali imetangaza bajeti ya Sh. trillioni 9.5 na karibu asilimia 34 zikiwa za tegemezi. Kilimo kimepangiwa matumizi yenye ukuaji wa asilimia 30. Nchini Uganda serikali imetilia mkazo maswala ya elimu, kilimo na kuondoa baadhi ya ushuru wa forodha kwa bidhaa kutoka nchi jirani - ikiwa ni ishara ya kutaka kuongeza biashara kati ya nchi hiyo na nchi za jirani.

Viongozi wa upinzani Tanzania hawakupendezwa na kwamba sehemu kubwa ya bajet hiyo ni ya tegemezi, wakati huko nchini Kenya baadhi ya wananchi wanadhani bajeti haijalenga ipaswavyo kuwasaidia wananchi wa kawaida.

XS
SM
MD
LG