Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 16:02

Marekani Yaitaka Israel Kusitisha Ujenzi wa Makazi Mashariki ya Kati


Akiwa ameambatana na mgeni wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Ahmed Gheit, Clinton alisema ucheleweshaji zaidi wa juhudi za kuleta amani Mashariki Kati utasababisha matatizo zaidi ndani na nje ya eneo hilo.

Waziri Clinton aliyasema hayo wakati juhudi za kidiplomasia zikiendelea kuhusu mgogoro wa Mashariki ya Kati, na Mjumbe wa Marekani katika eneo hilo, George Mitchell akiwa amefanya mazungumzo ya faragha na maofisa wa juu wa Israel mjini London.

Alhamis Rais Obama anatazamiwa kukutana na Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas.

Licha ya kwamba Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ambaye alitembelea White House wiki iliyopita hakufurahishwa na utaifa kamili wa Palestina, Clinton alisema kuwa yeye na Rais Obama wanania ya dhati ya kupata ufumbuzi wa mataifa mawili, na kwamba Misri ni mshirika muhimu katika kufanikisha hilo.

XS
SM
MD
LG