Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 26, 2020 Local time: 11:04

Uchaguzi wa Spika wa Bunge DRC


Mbunge wa jimbo la Kivu Kusini, Ditakwira Justin aliiambia Sauti ya Amerika kwa njia ya simu kuwa sababu kubwa ya kumuunga mkono spika wa zamani wa nchi hiyo Vital Kamerhe, ni kutaka kumwonyesha Rais Joseph Kabila kuwa hatakiwi kusikiliza tu watu wanaokubaliana naye katika kila jambo.

Justin alisema kuwa viongozi wa nchi hiyo wanataka watu ambao wanaitikia 'ndiyo' hata pale ambapo hawakubaliani na mawazo yaliyotolewa. Alisema imekuwa kama kanisani ambapo mchungaji akisema 'haleluya,' watu wote wanaitikia 'amina.'

Bwana Justin alisema kuwa wao kama wabunge wameungana pamoja wakitegemea kuwa (Rais Kabila) atawaita na kuongea nao, na hivyo wangeitumia nafasi hiyo kumweleza mawazo yao kuhusu kuheshimu katiba ya nchi hiyo na demokrasia.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG