Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:23

Viongozi wa G20 Wakubaliana Kuufufua Uchumi


Rais Barack Obama amesema mkutano wa mataifa 20 tajiri na yanayoinukia yanayojulikana kama G-20, ulofanyika huko London, utakua ni mwanzo wa mageuzi ya kuufufua uchumi wa dunia, baada ya kukubaliana kuimarisha masaada kwa mataifa maskini na kuweka masharti makali katika masoko ya fedha.

Bw Obama amesema mataifa ya G-20 yalkiweza kutanzua mivutano yao ya dhati na kufikia makubaliano ya kuimarisha ukuwaji wa uchumi, kubuni nafasi za kazi, na ku6toa mikopo kwa mataifa yanayokabiliwa na matatizo.

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown alisema viongozi walikubaliana Alhamisi huko Londo kuongeza kwa dola trilion 1.1 kwa mashirika makuu ya fedha na juhudi za kuimarisha uchumi wa dunia.

Mchambuzi wa masuala ya kuchumi mhadhiri wa chuo kikuu cha South Bank Huko London Dk Hilderbrand Shayo, anasema ni mafanikio makubwa hasa kwa vilekabla ya kuanza mkutano kulikua na wasi wasi juu ya namna viongozi wamegawanyika juu ya hatua za kuchukua.

Mataifa wanachama wa G-20 ni Argentina, Australia, Brazil, Canada, Uchina, Uingereza, Ufransa, Ujreumani, India, Indonesia, Italy, Japan, Mexico, Rashia, Saudi Arabia, Afrika Kusini, Korea ya Kusini, Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG