Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:30

Madagascar Yasikitika Kuodolewa Kutoka SADC


Ofisa wa ngazi ya juu katika serikali ya mpito nchini Madagascar anasema anasikitishwa na uamuzi wa Jumuiya ya Maendeleo kwa nchi za kusini mwa Afrika SADC, kusimamisha uanachama wa nchi yake katika jumuiya hiyo.

Waziri Mkuu Monja Roindefo aliiambia Sauti ya Amerika jana kuwa Madagascar huenda sasa ikajiondoa kutoka SADC kufuatia uamuzi huo. Roindefo alirudia tena maelezo yake kuwa serikali ya mpito nchini Madagascar siyo mapinduzi kwa sababu imehalalishwa na mahakama kuu ya nchi hiyo.

Mapema mwezi huu, Rais wa zamani Marc Ravalomanana alijiuzulu kutokana na shinikizo kali, na kukabidhi madaraka kwa jeshi la nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG