Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 16:47

Ndege Yaanguka Ziwa Victoria


Maofisa wa shirika la ndege la Uganda wanasema watu 10 wamekufa leo (Jumatatu) wakati ndege waliyokuwa wakisafiria ilipowaka moto na kuanguka katika Ziwa Victoria. Orodha ya wasafiri na wafanyakazi waliokuwemo ndani ya ndege hiyo bado haijatolewa, lakini maofisa wanasema kulikuwa na watu wapatao 10 au 11.

Maofisa wa jeshi la Burundi wanasema maofisa watatu wa vyeo vya juu katika jeshi la nchi hiyo, akiwemo Jenerali na Kapteni walikuwemo ndani ya ndege hiyo.Vyombo vya habari vya Russia vinaripoti kuwa rubani wa Russia, msaidizi wake, na injinia kutoka Ukraine ni miongoni mwa watu waliokufa katika ajali hiyo.

Uganda na Burundi zinachangia wanajeshi katika mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia. Maofisa wanachunguza chanzo cha ajali hiyo.

XS
SM
MD
LG