Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 12:09

Tsvangirai Katika Ajali ya Kawaida Barabarani


Wizara ya mambo ya nchi za njee imeeleza Jumapili kwamba lori lililogonga gari la waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai, siku ya Ijumaa ni la mradi wa pamoja wa kupambana na Ukimwi unaofadhiliwa na Marekani na Uingereza.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za njee alisema kwamba kila ishara inaonesha ajali ikua ya kawaida barabarani na hapakua na njama yeyote. Gari la waziri mkuu liligongana na lori moja kusini mwa mji mkuu waHarare na kusababisha kifo cha mkee wa Bw Tsvangirai.

Bw Tsvangirai amesafirishwa hadi Botswana ambako atapumzika na kufaraji baada ya kutolewa hospitali kufuatia ajali hiyo. Washauri wa karibu wa Bw Tsvangirai waliwambia waandishi habari kwamba waziri mkuu amechoka sana na anahitaji kupumzika.

Waziri wa fedha na katibu mkuu wa MDC Tendai Biti alisema Jumamosi kwamba pangelikua na polisi wanamshinikiza Waziri mkuu ajali hiyo ingeliweza kuepushwa.

XS
SM
MD
LG