Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 07, 2024 Local time: 00:47

Obama: Uchumi wa Marekani Utaimarika



Rais Barack Obama amesema Marekani itajikomboa kutoka hali ngumu ya uchumi na kuwa na nguvu zaidi kuliko ilivyo kuwa awali. Katika hotuba yake ya kwanza mbele ya kikako cha pamoja cha bunge rais alieleza kwa mapana sera zake za uchumi.

Akihutubia ukumbi uliojaa wabunge, maafisa wa serekali na wageni wa heshima, Rais Obama alisema, "sijaja hapa leo usiku kuwahutubia waheshimiwa wanaume na wanawake katika ukumbi huu bali kuzungumza kwa bayana na moja kwa moja kwa wanaume na wanawake waliotuleka hapa"

Rais Obama alisema kuwa baada ya muongo mzima wa sera za kiuchumi za kutojali, siku ya ukweli kwa Marekani imefika, na ni wakati wa kuchukua udhibiti wa mustakabali wetu hivi sasa.

Alisema "wakati uchumi unadorora imani zetu zimeshtuka kutokana na maisha magumu na wakati usio na uhakika, usiku wa leo ninataka kila Mmarekani afahamu kwamba tutakarabati, tutasalimika na Marekani itaibuka kuwa na nguvu kuliko ilivyo kuwa awali."

Bwana Obama alikiri kwamba kuna matatizo ya fedha na maamuzi magumu ya kuchukua lakini alisisitiza vipau mbele vinaweza kugharimiwa, ikiwa kutapunguzwa kwa busara mipango mingine kuanzia kilimo hadi ulinzi.


Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG