Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 19:46

Kenya: Bunge Kuunda Katiba Mpya


Bunge la Kenya limeunda kamati itakayokuwa na jukumu la kuunda rasimu ya katiba mpya katika kipindi cha miaka miwili.

Ababu Nambwamba, mbunge wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) amesema leo kuwa mabadiliko hayo ya katiba ni muhimu kuondokana na katiba ya sasa ambayo imekuwepo tangu enzi za utawala wa kikoloni.

Mbali na mabadiliko hayo ya Katiba, kamati hiyo itakuwa na jukumu la kuchunguza na kufafanua mipaka ya bunge, na pia kuunda tume itakayo simamia uchaguzi wa nchi hiyo.

Bwana Namwamba anasema msukumo zaidi wa kufanya mabadiliko hayo umekuja baada ya machafuko yaliyofuatia uchaguzi wa nchi hiyo Disemba 2007. Hata hivyo anasema wakenya wamekuwa wakidai mabadiliko hayo kwa muda mrefu.

XS
SM
MD
LG