Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 20:05

UN Kupeleka Walinda Amani Zaidi DRC


Baraza la usalama la umoja wa mataifa limekubaliana kupeleka polisi na wanajeshi wa kulinda amani 3000, kusaidia jeshi dogo la umoja huo mashariki mwa Congo.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika aliyepo makao makuu ya umoja huo mjini New York, Margaret Besheer, anasema baraza hilo limepitisha kwa sauti moja ombi la katibu mkuu wa umoja wa mataifa la kupeleka walinzi wa amani zaidi kwa muda.

Bado haijulikani ni mataifa gani yatachangia wanajeshi wake na ni lini jeshi hilo litawasili eneo lenye machafuko. Balozi wa Ufaransa Jean-Maurice Ripert amesema baadhi ya nchi zimekubali kuchangia wanajeshi, lakini kitengo cha kulinda amani bado kinaendelea kutafuta idadi kamili inayotakiwa na kwamba inaweza kuchukua wiki kadhaa.

Wanadiplomasia wanasema kusaidia MONUC nchini DRC ni hatua ya lazima kusaidia mpango dhaifu wa amani na kupunguza makali ya mgogoro wa kibinadamu.

Jeshi la kulinda amani la umoja wa mataifa nchini DRC ni kubwa kuliko yote duniani likiwa na walinda amani elfu 17.

XS
SM
MD
LG