Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 23:06

Migomo ya Wafanyakazi, Wanafunzi Tanzania


Mchambuzi wa masuala ya siasa amesema leo kuwa migomo ya wafanyakazi na wanafunzi nchini Tanzania itaendelea kama serikali ya nchi hiyo haitaongeza juhudi kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.

Profesa Xavier Lwaitama ameiambia Sauti ya Amerika kuwa migomo inaonekana kuwa mingi kwa sababu ya mivutano iliyopo kati ya serikali na waandamanaji. Ametoa mfano wa uamuzi wa serikali hivi karibuni kuzuwia migomo ya waalimu, walimu kutaka kumpiga kiongozi wao baada ya kuwaletea ujumbe kuwa wasingeweza kuendelea na mgomo wao, na pia hatua ya serikali kwenda mahakamani kwa lengo la kuzuwia migomo hiyo.

Profesa Lwaitama amesema serikali imekuwa ikijaribu kutafuta mchawi kwa kuwanyooshea vidole viongozi wa makundi hayo na vyama vya upinzani, hatua ambayo anasema haiwezi kusaidia kupata ufumbuzi mzuri wa tatizo hilo.

Kwa mujibu wa Profesa Lwaitama, migomo hiyo imekuwa mingi kutokana na tatizo la kiuchumi linalowakabili wananchi wengi, na malimbikizo ya fedha nyingi serikali ya nchi hiyo inadaiwa na wafanyakazi wa idara mbalimbali kama vile wafanyakazi wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika mashariki na walimu.

XS
SM
MD
LG