Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 00:29

Kenya Yaombwa Kufanya Uchunguzi wa Mateso kwa Wafungwa


Tume ya kitaifa ya haki za binadamu nchini Kenya imeiomba serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu vitendo vya mateso kwa wafungwa vinavyo dhaniwa kufanywa katika magereza ya nchi hiyo.

Mtetezi wa haki za binadamu kutoka kundi hilo Hassan Omar, ameiambia Sauti ya Amerika kuwa mateso kwa wafungwa nchini Kenya limekuwa jambo la kawaida, ambalo lilianza wakati wa utawala wa kikoloni na kuendelea baada ya nchi hiyo kupata uhuru wake.

Picha za video zilizochukuliwa hivi karibuni kwa kutumia simu ya mkononi zinaonyesha askari magereza wa Kenya wakiwapiga wafungwa kwa mikanda na fimbo, hatua ambayo inadhaniwa kupelekea kifo cha mfungwa mmoja.

Bwana Hasan anasema picha hizo zinathibitisha malalamiko ya muda mrefu ambayo yamekuwa yakitolewa na makundi ya kutetea haki za binadamu, na pia wananchi wa kawaida kuwa serikali ya Kenya inajihusisha na vitendo vya mateso kwa wafungwa.

Ameomba uchunguzi huru ufanyike kujua ukweli wa kifo cha mfungwa huyo na matukio mengine ya mateso kwa wafungwa yanayodhaniwa kufanywa na askari magereza.

XS
SM
MD
LG