Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 29, 2022 Local time: 23:52

Rice: Palestina Karibuni Kuwa Taifa


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice anasema uundwaji wa taifa la Palestina unakaribia, lakini akaonya kuwa mipango ya Israel kujenga makazi zaidi Ukingo wa magharibi inaathiri mazungumzo.

Rice aliyasema hayo baada ya kukutana na rais wa Palestina Mahmoud Abbas huko Ukingo wa magharibi. Rice amekiri kuwa makubaliano kati ya Israel na Palestina hayatafikiwa kwa muda uliokusudiwa mwishoni mwa mwaka huu, lakini amesema juhudi zitaendelea mwaka ujao katika utawala wa rais mteule Barack Obama.

Rice pia amekutana leo na viongozi kadhaa wa Israel, akiwemo waziri wa ulinzi Ehud Barak.

Waziri Rice amekuwa akikutana na viongozi wa Israel na pia rais wa Palestina Mahmoud Abbas kwa lengo la kutafuta amani ya mashariki ya kati na kuundwa kwa taifa la Palestina.

XS
SM
MD
LG