Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 20:35

UN Yaomba Mapigano Yasitishwe DRC


Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeomba mapigano yasitishwe mara moja katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo linasema mapigano mapya yanaweza kupelekea machafuko zaidi katika eneo zima la maziwa makuu.

Baraza hilo lenye wajumbe 15 lilisema jana kuwa lina wasiwasi sana na kurejea tena kwa machafuko katika eneo hilo na wasiwasi kuhusu madhara ya kibinadamu kutokana na machafuko hayo.

Lime laani pia wito wa hivi karibuni wa kiongozi wa waasi Jenerali Laurent Nkunda wa kutaka kuiangusha serikali iliyopo madarakani.

Nkunda alijiondoa kwenye mkataba wa amani ulio sainiwa mapema mwaka huu kwa maelezo kwamba serikali ya Congo imekuwa ikijadiliana kwa nia mbaya.

XS
SM
MD
LG