Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 07:50

Zuma Atoa Wito kwa Zimbabwe


Kiongozi wa chama tawala nchini Afrika Kusini amewaomba wana siasa wa Zimbabwe kufanya kazi kwa bidii ili kupata ufumbuzi wa kisiasa juu ya mkataba wa kushirikiana madaraka.

Jacob Zuma alisema kuwa alizungumza na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice kuhusu Zimbabwe wakati wa mkutano wao jana mjini Washington.

Alisema kuwa walikubaliana kuhusu haja ya kuzishinikiza pande zote mbili kukamilisha makubaliano.

Mazungumzo ya kushirikiana madaraka nchini Zimbabwe yamekwama kwa sababu wameshindwa kuelewana ni chama gani kitadhibiti wizara muhimu za serikali.

Juma tatu Marekani ilitishia kumuwekea vikwazo rais Robert Mugabe na watu wanao muunga mkono.

XS
SM
MD
LG