Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 06:47

Obama, Hillary Wafanya Mkutano wa Pamoja


Mgombea urais Marekani kwa tiketi ya chama cha Demokratic Barack Obama ameendelea na kampeni yake Florida leo ambapo kura za maoni za hivi karibuni zinaonyesha kuwa wagombea wote wa wili, Obama na mpinzani wake John McCain wana nafasi zuri ya kulinyakua jimbo hilo.

Seneta Obama amewaambia wafuasi wake kuwa kama akichaguliwa atahakikisha kuwa asilimia 95 ya wafanya kazi wanapata punguzo la kodi. Hatua hiyo, anasema itasaidia kuunda nafasi nyingi za kazi, hali ambayo itasaidia kuinua uchumi wa nchi.

Seneta Obama amewatahadhalisha wamarekani kuwa makini na hotuba na pia matangazo yanayotolewa na mpinzani wake kuwa anakusudia kuongeza kodi. Bwana Obama amesema wote, Obama na McCain wanakusudia kutoa punguzo la kodi. Laini akasema kuna tofauti kuhusu watu watakao pata punguzo la kodi.

Obama anasema sera yake yeye ni kuwapunguzia kodi wafanyakazi wa daraja la kati. Kwa upande mwingine, Obama anasema, McCain anaamini kuwa watu wanaostahili kupata punguzo la kodi ni wakurugenzi wa makampuni makubwa na makampuni yao, na siyo watu wenye kipato cha chini.

Mkutano huo pia ulihudhuliwa na seneta Hillary Clinton ambaye baada ya kumuunga mkono Obama katika mkutano mkuu wa chama cha Democratic, amekuwa akifanya kampeni katika majimbo yote muhimu kwa niaba ya Obama.

Akiongea katika mkutano huo, Seneta hillary amesema

XS
SM
MD
LG