Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 20:57

Hali ya Uchumi wa Kenya


Kenya ilikuwa moja ya nchi za Afrika zenye uchumi wenye nguvu katika miaka ya karibuni, huku kiwango cha ukuaji kikiwa ni asilimia tano tangu mwaka 2003 na ubashiri wa ukuaji ukiwa ni zaidi ya asilimia kwa mwaka huu wa 2008. lakini ghasia za kisiasa ambazo zimeua watu elfu moja na kuwakosesha makazi zaidi ya laki tatu tangu mzozo wa uchaguzi wa December, zimevuruga sana utendaji wa kiuchumi wa Kenya. Mwandishi wetu Derek kilner anaripoti.

Ukuaji unakadiriwa kwa mwaka 2008 kushuka kwa asilimia nne. Chama cha wazalishaji nchini Kenya kinasema ajira elfu 49 zitapotea, lakini idadi hiyo haijumuishi wengi ya watu waliokoseshwa makazi. Kama hawawezi kurejea majumbani mwao, mpaka ajira laki nne huenda zikawa katika hatari.

Utalii, sekta inayoongoza nchini Kenya, yenye mapato karibu dola bilioni moja mwaka 2007, umepigwa vibaya sana. watalii wanaowasili kwa robo ya kwanza ya mwaka 2008 wanatarajiwa kushuka kwa zaidi ya asilimia 91, huku mapato yakishuka kwa karibu dola milioni 80 kwa mwezi.

Kufanya mambo yawe mabaya zaidi, ghasia zimekuja katikati ya kipindi cha majira ya utalii, huku mahoteli kwenye ukanda wapwani na wafanyakazi katika setka yautalii wakitumia sehemu kubwa ya mapato yao ya mwaka.

Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya watalii nchini Kenya, ong’ng’a achieng anasema kwamba watu elfu 20 wamepoteza ajira, lakini athari zake zitahisiwa kila mahali.

“Tunaweza kuzungumzia elfu 20, lakini nadhani kuna wengi zaidi. Idadi hii tuliyonayo tumeipata kutoka kwenye mahoteli na nyumba za kulala wageni, lakini hatuzungumzii bajeti ya mahoteli na biashara nyingine zinazohusu utalii. Ni zaidi ya hayo.

Sekta ya utalii nchini Kenya imepitia vipindi vya matatizo hapo kabla. Lakini bodi ya utalii inasema changamoto ya sasa ni kubwa mno kuliko baada ya mashambulizi yakigaidi kwenye ubalozi wa marekani mjini Nairobi mwaka 1998 na kwenye hoteli inayomilikiwa na Israel kwenye pwani ya mombasa mwaka 2002.

Sekta ya maua nayo pia inashamiri sana Kenya na ni moja ya vipindi vyenye shughuli nyingi kabla kipindi hiki. Mji wa naivasha, kituo kikuu cha uzalishaji maua nchini Kenya, ulikuwa ni eneo la mapambano ya kutisha katika wiki za mwishoni za mwezi January ambayo yalizuia zaidi ya theluthi mbili ya wafanyakazi wake kufika kazini. Mkuu wa baraza la maua Kenya, jane ngige anasema asilimia 80 ya wafanyakazi katika sekta hiyo hivi sasa wako kazini, na hatua za muda zimechukuliwa kuruhusu mahitaji ya mauaji kutekelezwa. Lakini anasema mzozo unaleta hatari za muda mrefu kwa sekta hiyo, kama walivyo waagizaji na wasafirshaji ambao wanaangalia nchi nyingi kukidhi mahitaji.

XS
SM
MD
LG