Abiy alipokelewa na Rais Hassan Sheikh Mohamud na kuwa na mazungumzo yaliyohusu masuala ya amani na usalama, uchumi, diplomasia na uwezekano wa kushirikiana katika miradi ya pamoja na miundo mbinu.
Mivutano kati ya nchi hizo mbili ilizuka mwishoni mwa mwaka jana baada ya Ethiopia kufikia makubaliano na jimbo lililojitenga la Somaliland ili kupata njia ya kufika baharini.
Lakini Mogadishu na Addis Ababa zilifikia makubaliano ya kurudisha tena uhusiano wao wa kidiplomasia mwezi Januari kutokana na upatanishi wa Uturuki.
Katika taarifa ya pamoja baada ya mazunguzmo ya Alhamisi nchi hizo zimeleza kwamba ziara hiyo ilikuwa ni ya kuimarisha kuruidshwa tena ushirikiano kati ya majirani hao wawili.
Kufuatia kurudishwa kwa uhusiano huo hatma haijulikani tena ya mkataba wa Ethiopia na Somaliland.
Forum