Akilihutubia taifa Jumatano usiku kufuatia kutekwa kwa mji mkubwa kabisa wa mashariki wa Goma, Rais Tshisekedi alionya kwamba "kuna hatari kwa vita kugeuka kuwa vya kikanda."
"Kimya chenu na kutochukua hatua ni tusi kwa DRC," alisema kiongozi huyo akiongeza kwamba, kusonga mbele kwa wapiganaji wanaoungwa mkono na Rwanda kunaweza kupelekea moja kwa moja vita katika ukanda wa Maziwa Makuu.
Tshisekedi amesema kwamba jibu kali la kijeshi na lililopangwa liko njiani dhidi ya magaidi hao na wafadhili wao, akilalamika juu ya jinsi hali ya usalama ilivyozorota huko mashariki.
Hotuba yake imetolewa baada ya wapiganaji wa kundi la M23 kuteka miji miwili katika jimbo la Kivu Kusini siku ya Jumatano kufuatana na afisa wa serikali aliyezungumza na AFP.
Wakazi na maafisa wa miji ya Kiniezire na Mukwidja wanasema wapiganaji wa M23 hawakukabiliwa na upinzani wowote wakati wa asubuhi walipoteka miji yao.
Majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini, yenye utajiri mkubwa wa madini yenye thamani ya juu ,yamekua kati kati ya vita vya karibu miaka 30 vinavyo husisha makundi kadhaa yenye silaha, mara nyingi yakiungwa mkono na nchi jirani za Rwanda Burundi na Uganda.
Forum