Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 13:30

Bunge la DRC lamchagua Vital Kamerhe kuwa spika


Vital Kamerhe akihudhuria mkutano wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi ya Congo na waangalizi kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mjini Kinshasa.
Vital Kamerhe akihudhuria mkutano wa Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi ya Congo na waangalizi kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mjini Kinshasa.

Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilimchagua Vital Kamerhe, ambaye nyumba yake ilishambuliwa vibaya siku ya Jumapili, kuwa spika.

Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo lilimchagua Vital Kamerhe, ambaye nyumba yake ilishambuliwa vibaya siku ya Jumapili, kuwa spika katika kura iliyocheleweshwa, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea kuunda serikali miezi mitano baada ya uchaguzi wa rais.

Nafasi ya spika inamfanya Kamerhe, mshirika wa karibu wa Rais Felix Tshisekedi, kuwa mtu wa pili mwenye mamlaka katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

Kati ya wabunge 407 waliopiga kura siku ya Jumatatu, 371 walipiga kura kumuunga mkono Kamerhe kugombea uspika. Wabunge pia walitazamiwa kuwapigia kura wagombea wa nyadhifa nyingine sita katika baraza kuu la bunge.

Forum

XS
SM
MD
LG