Kulingana na maelezo rasmi ya matukio, watatu hao waliungana pasipo kutarajiwa chini ya uongozi wa kiongozi wa upinzani Christian Malanga, ambaye alijishughulisha na biashara ya uchimbaji dhahabu na magari yaliyotumika kabla ya kumshawishi mwanawe mzaliwa wa Utah kujiunga na jaribio la mapinduzi.
Watu sita, akiwemo Malanga, waliuwawa katika shambulio hilo mapema Jumapili na Wamarekani watatu walikuwa miongoni mwa darzeni ya watu waliokamatwa. Maafisa wanasema wanajaribu kufahamu ni jinsi gani mtoto wa Malanga mwenye umri wa miaka 21, Marcel, alivyotoka kucheza mpira shule ya sekondari hadi kudaiwa kujaribu kumn’goa madarakani kiongozi wa mojawapo ya nchi kubwa zaidi barani Afrika. Mama yake Marcel anasema mwanawe hana hatia.
Ubalozi wa Marekani mjini Kinshasa ulisema unafahamu raia wa Marekani huenda walihusika katika matukio ya Jumapili, akiongeza katika taarifa kwamba itashirikiana na mamlaka inapochunguza vitendo hivi vya uhalifu wa kikatili.
Forum