Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 08:08

Walinzi wa pwani Italia wawaokoa wahamiaji 37

FILE -Boti ya walinzi wa pwani ya Italia ikiwa imebeba wahamiaji waliookolewa baharini ikipita katikati ya boti za utalii, katika kisiwa cha Sicilian, Lampedusa, Italia, Sept. 18, 2023.
FILE -Boti ya walinzi wa pwani ya Italia ikiwa imebeba wahamiaji waliookolewa baharini ikipita katikati ya boti za utalii, katika kisiwa cha Sicilian, Lampedusa, Italia, Sept. 18, 2023.

Walinzi wa Pwani wa Italia Jumatano wamewaokoa wahamiaji 37 kutoka kwenye boti ya mbao.

Boti hiyo ilikuwa ikisafiri katika hali mbaya ya hewa kusini mashariki mwa Lampedusa.

Wahamiaji, ambao walikuwa wakisafiri kwenye boti yenye urefu wa mita saba, baadaye walifikishwa katika hali ya usalama kwenye kisiwa cha Italia.

Katika operesheni nyingine, mlinzi wa pwani wa Italia alitoa msaada kwa mamlaka ya kutafuta na uokoaji ya Malta.

Boti ya uokoaji ya Medicins Sans Frontiers (MSF) ikiwa karibu na boti ya mpira iliyobeba wahamiaji kutoka Mashariki ya Kati na Afrika, Juni 24, 2023. MSF/Skye McKee/Handout via REUTERS
Boti ya uokoaji ya Medicins Sans Frontiers (MSF) ikiwa karibu na boti ya mpira iliyobeba wahamiaji kutoka Mashariki ya Kati na Afrika, Juni 24, 2023. MSF/Skye McKee/Handout via REUTERS

Mamlaka hiyo ilikuwa imejibu ajali ya boti ndogo iliyozama kwenye maji ya Malta kiasi cha kilometa 50 kusini mashariki mwa Lampedusa.

Boti ya doria ya Italia iliwaokoa watu 22 na kupata miili tisa, akiwemo mtoto mdogo wa kike.

Forum

XS
SM
MD
LG