Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 19:58

Migogoro na mapinduzi yagubika mkutano wa 44 wa mawaziri wa Afrika


Makao Makuu ya Umoja wa afrika Addis Ababa.
Makao Makuu ya Umoja wa afrika Addis Ababa.

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Afrika wanakutana mjini Addis Ababa kwa mkutano wao wa 44 kutayarisha mkutano wa kilele wa 37 ambao viongozi watajadili suala la mfumo wa elimu barani humo pamoja na migogoro ambayo inasababisha hali ya ya wasi wasi katika sehemu nyingi za bara hilo.

Mawaziri wameanza mkutano kwa kutoa wito wa kuimarishwa juhudi za kuhakikisha utulivu barani humo na kuimarisha kiwango cha elimu.

Mkutano wa viongozi utaanza Jumamosi, tarehe 17 Februari ukigubikwa zaidi na suala la mapinduzi ya Gabon, Burkina Faso, Mali na Nigeri na hali ya kisiasa nchini Senegal, ikiwa ni miongoni mwa changemoto zinazo ukabili umoja huo unaojaribu kuongeza sauti yake kwenye jukwa la kimataifa.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika Moussa Faki Mahamat, akihutubia mkutano wa Mabadiliko ya Hali ya hewa.
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika Moussa Faki Mahamat, akihutubia mkutano wa Mabadiliko ya Hali ya hewa.

Akihutubia mkutano wa Baraza la Utendaji la mawaziri wa mambo ya nje, mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Moussa Faki Mahamat, alisisitiza juu ya haja ya kuongeza juhudi ili kuhakikisha amani na usalama unadumishwa pamoja na maendeleo ya kiuchumi na kijami yanapatikana na wanachama kugharimia kwa uendelevu AU pamoja na kuimarisha mfumo wa ushirikiano ya kimataifa.

"Kujitokeza upya mapinduzi, ghasia za kabla na baada ya uchaguzi, mizozo ya kibinadamu inayoambatanishwa na vita au athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa pamoja ni mambo yanayobidi kututia wasi wasi sote. Matatizo hayo ni hatari kubwa katika kuharibu ishara za ukuwaji wa Afrika ambao tunajivunia," lisema Mussa Faki Mahamat.

Wakosoaji wa umoja huo wanasema mizozo ya karibuni katika bara la Afrika imefichua changamoto zilizopo kukabiliana na wimbi la mapinduzi huko afrika magharibi, vita vya takriban mwaka mmoja vya Sudan na kuongezeka kwa mivutano mashariki mwa DRC ambayo inatishia migogoro kati ya nchi na nchi katika mkanda hiyo.

Kutatua haya mshauri mwandamizi wa kundi la kimataifa la utatuzi wa migogoro- ICG, Liessl Louw –Vaudran amesema AU ina wajibu wa kuzungumza wazi kama uchaguzi una kasoro na sio wakuaminika .

“Kwa hiyo kitu kimoja tunasema katika ripoti yetu ni kwamba, tunapoona kuna changamoto za kiutawala uchaguzi usio huru na sawa AU sio tu ifuatilie na kutoa ripoti, na katika lugha ya kidiplomasia: kwa hiyo unajua , kulikuwa na changamoto za kiufundi. inatakiwa kuzungumza wazi kuhusu uchaguzi uliokuwa na wizi kwa sababu tunaona hiyo ni moja ya sababu za mapinduzi ya kijeshi,” amesema Liessl Louw-Vaudran

Mkutano wa siku mbili unawaleta pamoja mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 54 wanachama wa AU ukifanyika chini ya kauli mbiyu elimu itakayoifaa Afrika katika karne ya 21, kwa kubuni mifumo ya elimu stahmilivu inayoongeza uwezo wa kuwaruhusu kila mmoja kupata elimu inayostahiki Afrika. Mawaziri wanatayarisha mkutano wa 37 wa siku wa viongozi utakaoanza Jumamosi.

Takwimu za AU zinaonesha kwamba idadi ya watoto waloacha shule imefikia milioni 98 huko Afrika na kiwango cha watoto wasioweza kusoma na kuandika katika nchi za Afrika kusini mwa janga la Sahara inakadiriwa kufikia asili mia 90.

Forum

XS
SM
MD
LG