Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 23, 2026 Local time: 02:50

Watu 30 wakamatwa wakishukiwa kuuza watoto wachanga Morocco

Jiji la Fez huko Morocco. Picha na FADEL SENNA / AFP
Jiji la Fez huko Morocco. Picha na FADEL SENNA / AFP

Polisi nchini Morocco wamewakamata watu 30 wanaoshukiwa kuhusika na biashara haramu ya watoto wachanga katika mji wa kaskazini wa Fez, Shirika la habari la serikali limeripoti

Miongoni mwa waliokamatwa ni walinzi 18, daktari, wauguzi wawili na maafisa wengine wa afya pamoja na madalali, Shirika la habari la Moroco MAP limeripoti Jumatano usiku, likinukuu chanzo cha usalama.

Hawakutoa idadi halisi ya watoto wanaodaiwa kusafirishwa.

Idadi ya waliokamatwa wanashukiwa “ni madalali katika kuuza watoto wachanga kutoka kwa akina mama wasio na waume…. kwenda kwenye familia zinazotaka kuasili watoto waliotelekezwa” kimesema.

Operesheni hiyo iliyofanywa na polisi wa Fez wakishirikiana na idara ya ujasusi ya Morocco pia walikamata “dawa zilizoidhinishwa na daktari, dawa ambazo haziuzwi, vifaa vya matibabu and kiasi cha fedha” kutoka katika nyumba za washukiwa.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

This item is part of

Forum

​
XS
SM
MD
LG