Wabunge wa Marekani wanaweka wazi uwezekano wa kufikia makubaliano ya msaada kwa Ukraine, kabla ya kuondoka mjini Washington kwa likizo ya sikukuu wiki ijayo.
Maseneta wa Marekani waliendelea na mazungumzo Alhamisi mchana kuhusu ombi la White House, la usalama wa taifa lenye thamani ya dola bilioni 106, ambalo linajumuisha msaada wa kijeshi na kibinadamu wa dola bilioni 60 kwa Ukraine.
Maseneta wa Republican wamewasilisha pendekezo lao la ufadhili wa usalama wa mpakani na mabadiliko ya sheria ya uhamiaji ya Marekani, kwa ajili ya kurejesha kura zao zinazoidhinisha duru mpya ya msaada kwa Ukraine. Baraza la Seneti lilipanga Alhamisi kuondoka katika kikao kilichosalia cha mwaka.
Kiongozi wa walio wengi katika baraza la seneti, Chuck Schumer anatarajiwa kutangaza kuwa bunge hilo litaahirishwa kwa ajili ya wikiendi, na kurejea kazini kwa mashauriano siku ya Jumatatu
Forum