M-misionari mmoja raia wa Ujerumani, Father Hans Joachim Lohre ambaye alitekwa nyara katika mji mkuu wa Mali, Bamako mwaka jana ameachiwa huru na mtekaji wake, afisa wa kanisani ameliambia shirika la habari la Reuters siku ya Jumapili.
Patient Nshombo wa Missionaries for Africa ameliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu kwamba Lohre ameachiliwa huru. Ndiyo, ameachiliwa huru, lakini tunapaswa kusubiri maelezo zaidi kutoka kwa mamlaka, alisema Nshombo.
Serikali ya Mali haikujibu mara moja ombi la kutoa maoni juu ya tukio hilo. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani amekataa kutoa maoni yake. Lohre, ambaye alikuwa akiishi Bamako kwa miaka 30 alitarajiwa kuhudhuria Misa ya Jumapili asubuhi katika mji mkuu wa Mali hapo mwaka jana wakati wenzake walipogundua kwamba gari lake lilikuwa lime-egeshwa mbele ya nyumba yake na simu yake ilizimwa.
Forum