Rais mteule wa Argentina, Javier Milei alisafiri Jumapili kuja Marekani kukutana na maafisa wa Marekani na wa kimataifa, vyanzo vya kidiplomasia vimeliambia shirika la habari la AFP.
Mchumi huyo wa siasa kali za mrengo wa kulia, atawasili mjini New York kwa ziara ya kibinafsi siku ya Jumatatu, kabla ya kusafiri siku hiyo-hiyo kwenda Washington, ambako atakutana na mwanadiplomasia wa Marekani Juan Gonzalez, vyanzo hivyo vimeliambia shirika la habari la AFP, kwa sharti la kutotajwa jina.
Gonzalez ni naibu waziri wa mambo ya nje wa masuala ya Western Hemisphere. Ajenda ya Milei hadi siku ya Jumanne pia inajumuisha mazungumzo na maafisa wa Wizara ya Fedha, vyanzo hivyo vimesema.
Milei atawasili na wanachama kadhaa wa timu yake akiwemo Luis Caputo, mshauri wa masuala ya kifedha ambaye anaonekana atakuwepo kama mwanachama katika baraza la mawaziri.
Forum