Mkanyagano katika uwanja wa kijeshi umesababisha vifo vya watu wasiopungua 37 huko Jamhuri ya Congo baada ya umati mkubwa wa vijana kuitikia wito wa kuandikishwa, mamlaka imesema Jumanne.
Mwendesha mashtaka wa umma Oko Ngakala alisema uchunguzi utaanzishwa na kuhoji kwa nini tukio hilo lilikuwa bado linaendelea hadi usiku wa manane. Brandon Tsetou, kijana msomi ambaye alikimbia msongamano huo, alisema alikuwa amepanga mstari mbele ya uwanja wa Ornado tangu Jumatatu asubuhi. “Kulingana na waandaaji ilikuwa siku ya mwisho.
Ndio maana wengi wetu tuliamua kusubiri hadi usiku wa manane, tukiwa na matumaini ya kujiandikisha”, aliliambia shirika la habari la Associated Press. “Baadhi ya watu walikuwa walikosa subira na kuamua kuingia ndani kwa nguvu, na hivyo kutoeka mkanyagano uliosababisha watu kadhaa kufariki dunia au kujeruhiwa, jambo ambalo linasikitisha”.
Forum