Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 16:15

Picha za wafanyakazi 41 wa India waliokwama kwenye handaki zimeonekana

Timu ya waokoaji ikiwa imesimama kwenye lango kuu mahala ambapo wafanyakazi wa ujenzi wa barabara wamekwama huko Uttarkashi
Timu ya waokoaji ikiwa imesimama kwenye lango kuu mahala ambapo wafanyakazi wa ujenzi wa barabara wamekwama huko Uttarkashi

Wafanyakazi hao walikuwa wakijenga handaki hilo kama sehemu ya mradi wa barabara kuu katika milima ya Himalaya ambalo sehemu moja ilianguka hapo Novemba 12.

Nchini India picha za kwanza za wafanyakazi 41 wa ujenzi waliokwama katika handaki kwenye jimbo la kaskazini la Uttarakhand zilionekana leo Jumanne wakati timu za uokoaji zilipoanzisha mawasiliano ya kuonana nao.

Wafanyakazi hao walikuwa wakijenga handaki hilo kama sehemu ya mradi wa barabara kuu katika milima ya Himalaya ambalo sehemu moja ilianguka hapo Novemba 12.

Video iliyotolewa na mamlaka ya jimbo inaonyesha wanaume hao wakiwa wamevaa kofia ngumu za kazi na makoti ya ujenzi na kusimama karibu na kamera ya utafiti wa matibabu ambayo ilitumwa kupitia bomba lenye urefu wa mita 15 lililopelekwa kupitia kifusi siku ya Jumatatu.

Afisa alionekana akiwaomba wanaume kutabasamu na kunyanyua mikono yao. Ambapo wafanyakazi hao walionekana wanaweza kuitikia maagizo wanayopewa.

Forum

XS
SM
MD
LG