Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 25, 2025 Local time: 16:30

Wafuasi wa upinzani Senegal wanalaani ukatili uliokithiri unaofanywa na polisi


Vyombo vya usalama Senegal vikikutana na waandamanaji wa upinzani nchini. Dakar, June 3, 2023.
Vyombo vya usalama Senegal vikikutana na waandamanaji wa upinzani nchini. Dakar, June 3, 2023.

Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Senegal, Ousmane Sonko wanalaani ukatili uliokithiri unaofanywa na polisi siku ya Jumapili baada ya majibizano kuhusiana na hukumu yake ya hivi karibuni ya kifungo cha jerla na kusababisha vifo vya watu 16 na zaidi ya waandamanaji 350 kujeruhiwa.

Ghasia hizo zilizuka Alhamisi wakati Sonko alipohukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani katika kesi ambayo anasema ililenga kumzuia kuwania urais nchini humo mwaka ujao. Shirika la Msalaba Mwekundu limesema limewasaidia waandamanaji 357 waliojeruhiwa akiwemo mwanamke mjamzito pamoja na askari 36 wa maafisa wa ulinzi na usalama waliojeruhiwa tangu ghasia zilipozuka.

Kwa ujumla watu 78 waliojeruhiwa vibaya walipelekwa katika vituo vya afya, iliongeza taarifa hiyo. Wafuasi wa Sonko na Rais Macky Sall wanatupiana lawama kwa ghasia na vifo hivyo. Siku ya Jumapili, chama cha Sonko cha PASTEF-Patriots kililaani ukandamizaji wa mauaji unaofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama, kiki-ishutumu serikali kwa kupeleka wanamgambo binafsi.

Forum

XS
SM
MD
LG