Mbunifu raia wa Scotland na Ghana Lesley Lokko anakabidhi jukwaa kwa sauti ambazo zimenyamazishwa kwa muda mrefu katika maonyesho ya mwaka huu ya Usanifu ya Venice maarufu kama Venice Architecture Biennale.
Maonysho hayo yaliyofunguliwa Jumamosi ikiwa ni ya kwanza kuwahi kuratibiwa na Mwafrika, yakishirikisha kazi nyingi za Waafrika na wale wanaoishi nje ya nchi.
Maonyesho hayo ya Biennale ya 18 ya usanifu, yaliopewa jina la The Laborator of the Future, yanaangazia kuondoa ukoloni na kuondoa wa hewa chafu mada ambazo Waafrika wana mengi ya kusema, Lokko alisema, akitoa mfano wa unyonyaji wa muda mrefu katika bara hilo na kwa rasilimali watu na mazingira.
Mwili mweusi ulikuwa kitengo cha kwanza cha nishati barani Ulaya, Lokko aliliambia shirika la habari la Associated Press wiki hii. Tumekuwa na uhusiano kwa rasilimali tangu zamani. Tunafanya kazi mahali ambapo rasilimali si thabiti. Pia mara nyingi ni tete. Mara nyingi hutumiwa. Uhusiano wetu nao ni wa kinyonyaji.