Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 12:56

Watu 33 wauwawa na washukiwa wafuasi wa itikadi kali Burkina Faso

Raia wa Mali wakivusha ng'ombe Mto Niger kwenye Bandari ya Korioume, kusini mwa Timbuktu, Mali, Feb. 3, 2013.
Raia wa Mali wakivusha ng'ombe Mto Niger kwenye Bandari ya Korioume, kusini mwa Timbuktu, Mali, Feb. 3, 2013.

Shambulio lililofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa itikadi kali za Kiislamu kwenye kijiji kimoja magharibi mwa Burkina Faso liliua raia 33, ofisi ya gavana wa jimbo hilo ilisema.

Shambulio lililofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa itikadi kali za Kiislamu kwenye kijiji kimoja magharibi mwa Burkina Faso liliua raia 33, ofisi ya gavana wa jimbo hilo ilisema.

Idadi ya vifo vya awali kutokana na shambulio la Alhamisi jioni kwenye kijiji cha Youlou katika mkoa wa Mouhoun ilitangazwa katika taarifa kwenye vyombo vya habari.

Gavana wa jimbo hilo Babo Pierre Bassinga alitaja shambulio hilo kuwa la uoga na la kinyama. Alisema katika taarifa hiyo kuwa shambulio hilo lilitokea majira ya saa 11 jioni wakati wakazi walipokuwa kazini katika mashamba yao kando ya mto Mouhoun. Gavana huyo alisema hatua za kiusalama zinaendelea ili kukabiliana na itikadi kali.

Bassinga aliwataka wananchi kuongeza umakini wao na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.

XS
SM
MD
LG