Uturuki inapiga kura katika uchaguzi wa rais na bunge Jumapili, katika kile kinachotabiriwa kuwa mojawapo ya uchaguzi wenye ushindani mkubwa zaidi katika miongo kadhaa na mojawapo ya kura muhimu zaidi, ndani ya nchi na kimataifa. Kura hiyo itaamua hatima ya kisiasa ya Rais Recep Tayyip Erdogan, ambaye ametawala kwa zaidi ya miaka 20.
Uchaguzi wa Jumapili unatabiriwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kupiga kura katika nchi yenye mojawapo ya viwango vya juu zaidi vya ushiriki wa upigaji kura duniani. Wote wawili Rais aliye madarakani Erdogan na mpinzani wake mkuu, Kemal Kilicdaroglu, wanadai uchaguzi huo ni muhimu zaidi katika historia ya nchi hiyo.
Katika wilaya ya Kadikoy ya Istanbul, upigaji kura ulienda kwa haraka, kuanzia vituo vya kupigia kura vilipofunguliwa. Uchumi ndio ulikuwa wasiwasi mkuu kwa mpiga kura Mustafa, ambaye alitaka tu kutambuliwa kwa jina lake la kwanza.